Breaking News

NDOTO

NDOTO
Mungu hutumia ndoto kama njia ya kusema na mtu  ni kumjulisha yalliyo kusudiwa inaweza kuwa kuhusu ufalme wa Mungu,ufalme wa giza (kuzimi) na duniani pia.
*    1wafalme 3:5-15
Mara nyingi Mungu husema na watu au mtu kupitia ndoto ila watu hawajajua kuwa Mungu anawapa maelekezo wao huupuzia na kuona ni kawaida.
*    Mwanzo 15:1
Mara nyingi ndoto hutoa picha ya mambo yatakayo tokea kwa mtu .mfano mtu anaota msiba lakini inatokea kwenye ulimwengu wa mwili kama alivyoota.
VIGEZO VYA MUNGU KUMKUBALI MTU
1.Inategemea ntu amejitoa kwa kiasi gani kwake Mungu.
2.Inategemea mtu anakuwa kwa kiwango gani katika Mungu.
Mungu hukuza watoto wake kwanjia mbalimbali moja wapo ni ndoto.
LENGO KUU LA MUNGU KUZUNGUMZA KUPITIA NDOTO
1.Ni njia rahisi ya Mungu kusema na mtu
*    Mwanzo 15:1
2.Hutumia ndoto kuzungumza na mtu kwa sababu watu wengine ni waoga kwa hiyo Mungu hawezi kusema nao kwa njia ya wazi.
3.Ni kumpatia mtu ramani ya safari anapo kuwa duniani.
4.Ni kumpatia ufahamu mtu juu ya kuenenda duniani n.
Ndoto inapo kuja kwa kujirudarudia mara nyingi ni picha ya tukio liko kalibu kutokea.
*    Yohana 3:8-
*    Mithali 1:6
Hakikisha unapoota ndoto unaiandika hiyo ndoto haijalishi ni mbaya au ni nzuri.
Sababu za kuandika ndoto.
1.Inawezekana kwa wakati huo unaota hiyo ndoto bado ni mchanga kiroho kwahiyo  utakapo kuwa itasaidia kumkumbusha Mungu juu ya lile jambo alilosama na wewe.
2.Ili kuwa na nguvu ya maombi na ili kuruhusu upako wa maombi.
*    Habakuki 2:1-2
Kuna ndoto zingine zinatokana na shughuli za mtu alizozifanya mchana kutwa au mwazo ambayo mtu anawaza kwa muda mrefu.
Changamoto shetani akijua kuwa mtu aliye moyoni kwa mtu nani msada wa huyo mtu hutumia picha ya mtu huyo kwa namna iliyo mbaya ili kuvunja imani juu ya mtu unayemtengemea (kuleta faraka).
Mtu ukiota Mtumshi au mtu aliye ndani ya moyo wako anakusaidia sehemu Fulani inapaswa kushukuru na kumuombea ulinzi na ukiota jambo baya  vilevile anza kumuombea ndipo Bwana ataanza kushulika na pepo anaye halibu ufahamu wako.


No comments